Je,upo udhaifu katika kudhibiti madawa ya kulevya kwa vijana? sehemu ya 2


ATHARI  za madawa ya kulevya ,matumizi yake na usafirishwaji wake, imeonekana kazi hiyo kwa asilimia kubwa ikifanywa na vijana  hali inayoelezwa inatokana na vijana kuwaka tamaa ya utajiri wa haraka katika umri mdogo, pia baadhi yao wamekata tamaa ya kutokana na ugumu wa maisha,lakini wapo wengine wanatumia madawa hayo kama (fashion)wanaiga kutokana na makundi na mazingira yanayowazunguka.

LAKINI vijana wengi na wadau mbalimbali wamekuwa na malalamiko juu ya serikali ,kwa kudai kwamba kitengo maalum cha kudhibiti madawa hayo,hakitendi kazi yake ipasavyo hali inayopelekea kuwe na udhaifu katika udhibiti hali ya ya matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana kundi ambalo ndilo linaonekana kuathrika kwa wingi na madawa hayo ya kulevya. Continue reading

Advertisements

Jinsi ulevi unavyomuathiri kijana


Ulevi uliokithiri umeonekana kuwa ni janga ambalo linawaangamiza vijana kwa wingi na kusababisha hali ya uchumi ya vijana hao kuporomoka kiuchumi hali inayotishia maisha yaona taifa kwa ujumla, mambo kama hayo kwa kijana ambaye anategemewa na familia yake , ulevi umeonekana kuwaathiri vijana wengi na kupelekea familia zao zinazowategemea kuwa katika hali ngumu ya kiuchumi.

Maoni hayo yametolewa na wadau mbalimbali ,wanaharakati wa haki za vijana,pamoja na wataalamu wa afya, ambapo imeonekana kijana anapotumia kilevi ,haijalishi iwe ni pombe ya kawaida au pombe kali,maarufu kwa jina la (gongo), anashindwa kuzidumu vizuri akili zake na kujikuta akitenda mambo ya ajabu katika jamii inayomzunguka,kama vile ugomvi, kuwaka tamaa za mwili,ubakaji na mengine mengi yanayosababishwa na ulevi wa pombe.Dr mwanjela wa Muhimbili alikuwa na haya ya kusema; Continue reading

Je, upo udhaifu katika kudhibiti madawa ya kulevya kwa vijana? sehemu ya 1


Mfano wa madawa ya kulevya yanayowaathiri vijana kwa wingi nchini (picha kwa hisani ya global publishers)

SAKATA la utumiaji madawa ya kulevya na uwepo  wake kwa wingi nchini hasa kwa vijana ambao ndio watumiaji wakubwa wa madawa hayo,limeonekana likizidi kukuenea na kuendelea kutapakaa kila pembe ya nchi ya Tanzania licha ya kuwepo kitengo maalum cha udhibiti wa madawa ya kulevya nchini, kilichoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya tisini na kuanza kazi rasmi mwaka 1995,hadi sasa imetimia miaka 11 ya kuanzishwa kwake  lakini bado tatizo hilo linazidi kukua kwa kasi kubwa.Wadau mbalimbali na vijana hapa nchini wamekuwa na maoni tofauti juu ya kitengo hicho cha udhibiti wa madawa ya kulevya nchini, kinachoongozwa na Kamanda Godfrey Nzowa, kitengo hicho kimekiri kuwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kupambana na madawa ya kulevya.

TUME  ya taifa ya kudhibiti madawa ya kulevya nchini walisema tatizo kama hilo wanalishughulikia kwa kuandaa semina na warsha mbalimbali za kuwaelimisha vijana juu ya masuala hayo  ya utumiaji wa madawa ya kulevya yanavyowaathiri vijana na yanavyoweza kuwaharibia maisha vijana hao na kuwasababisha wengine hata kupata magonjwa ya akili katika kichwa chao.Hivyo kumaliza tatizo hilo wanahitaji ushirikiano mkubwa toka kwa wananchi wote kwa ujumla.Kamishina wa Tume ya kuratibu na kudhibiti madawa ya kulevya nchini,Shekiondo Christopher Continue reading