Vijana tanzania na soko huru la A. Mashariki sehemu ya 2


Starehe pia na ulevi limeonekana ni tatizo linawakumba watanzania wengi mda wa kazi wanaacha kuendelea na kazi kwenda  kufanya starehe mda wa kazi na kusahau mda huo ni wa kazi na sio mda wa kufanya starehe,hali hiyo nayo imekuwa kama chachu kwa vijana hawa kuweza kufurukuta katika soko la Afrika mashariki,Bi,Zahara,mkurugenzi wa makampuni mbalimbali yanayohusika na uzlishaji alikuwa na haya ya kusema:

“Uvivu ni tatizo hasa maana mda wa kazi unakuta mtu yupo amesinzia au anaongea na simu mda mrefu na kusahau kuwa yupo kazini, asubuhi mapema mtu yuko ‘facebook’ au ‘yahoo messenger’anachati na kuacha kufanya kazi eti kisa kuna mtandao wakati mi nimeweka mtandao wa kazi ,na pia vijana wengi wa kitanzania sio waaminifu mtu ukimuamini siku mbili hakawii kukuibia na kutoka na wakati mwingine anakuwa sio mwaminifu katika biashara unyompa kufanya,kwa hali hiy mimi naona watashindwa kulimudu soko huru la Afrika mashariki”. Continue reading

Advertisements

Vijana tanzania na soko huru la A. Mashariki sehemu ya 1


Uvivu  na  kutopenda kujituma ni hali ambayo imeonekana ikileta ugumu kwa vijana wengi wa Tanzania kuleta ushindani wa soko huru la Afrika mashariki lilifunguliwa mnamo mwezi juni mwaka 2011 ili kuruhusu nchi za Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi na Tanzania katika kushirikiana mambo mbalimbali ya kiuchumi  ili kukuza uchumi wa pamoja wa Afrika mashariki.

Hali hiyo imeweza kujionesha katika makampuni mbalimbali wageni kutoka nje ya nchi kama Kenya na Uganda kupewa kipaumbele zaidi katika ofisi mbalimbali na kumiliki nafasi za juu za uongozi huku vijana wa kitanzania wakibaki kushika nafasi za chini sana kama usekretari,mesenja na ufagiaji wa maofisini hali ambayo imekuwa ikiwaumiza vijana wengi wa kitanzania lakini mkurugenzi mmoja wa kampuni ya masoko(jina linahifadhiwa) alikuwa na haya ya kusema. Continue reading