Watuhumiwa madawa ya kulevya waburuzwa kortini


Sakata la madawa ya kulevya, watuhumiwa wengi wamefikishwa kortini na kutokana na shria za nchi watakaopatikana na makosa watapewa adhabu ya kifungo cha miaka 20 au fidia mara tatu ya mzigo waliokamatwa nao.

Hata hivyo, hakimu mmoja aliyehojiwa na mwandishi huyu alisema watuhumiwa waliokamatwa ni wale vijana wadogo wado lakini wafanyabiashara wakubwa bado hawajapatikana hasa ikikumbukwa kuwa vijana hao hawakubali kuwataja wakubwa wanaohusika kuingiza madawa hayo kutoka nchi zanje kama Pakistan.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, watuhumiwa hao wanapofikishwa mahakamani askari wa kitengo cha madawa ya kulevya hawahusiki tena katika kutoa hukumu au kuwa na sauti katika jambo hilo bali wanasubiria hukumu ya hakimu katika kesi hizo za watuhumiwa hao.

Katika ufuatiliaji wa kesi hizo umeonekana kwamba kesi nyingi za madawa ya kulevya hupelekwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu na mahakama ya karikoo katika kutolea hukumu kesi hizo za madawa ya kulevya. Continue reading

Advertisements