Tuhuma za ‘UGAIDI’ zamfikisha mahakamani Lwakatare wa Chadema.


Rwakatare

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka manne likiwamo la kula njama ya kutaka kutoa sumu, kufanya mkutano wa ugaidi na kupanga tukio la kumteka nyara Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.

Lwakatare na mwenzake, Ludovick Rwezaula, walifikishwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana saa 2:00 asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Akiwasomea washtakiwa hao mashitaka yao, Wakili Rweyongeza alidai kuwa
Desemba 28, mwaka 2012, katika eneo la King’ongo, Kimara Stop Over, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja, walikula njama ya kutenda kosa la jinai kwa nia ya kumdhuru Dennis Msacky kwa kumpa sumu.
Washtakiwa wote kwa nyakati tofauti walikana mashitaka hayo.

Wakili huyo alidai kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ugaidi namba 20, mashitaka yanayowakabili washtakiwa hayana dhamana na kwamba upelelezi utakapokamilika kesi hiyo itaendeshwa katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Upande wa utetezi uliongozwa na Mawakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu, Peter Kibatala na Nyaronyo Kicheere.
Lwakatare na mwenzake, waliokuwa kwenye gari yenye namba za usajili T 140 BLA aina ya Land Cruiser rangi nyeupe, waliondolewa kwenye viunga vya mahakama hiyo huku wakiwa kwenye ulinzi mkali wa magari ya Jeshi la Polisi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s