About us

HI,Karibuni sana vijana na watu wote katika sehemu maalumu ya vijana kukutana na kutoa mawazo yao mbalimbali, na pia  kupata habari muhimu za mambo yanayowahusu  vijana kila siku katika mambo ya kiuchumi,kiutamaduni,kielimu,kimichezo ,kisiasa na mengine mengi ili kuweza kumfanya kujitambua na kutimiza majukumu yampasayo kufanya ili kutimiza malengo yake katika kulijenga taifa letu

Karibuni waungwana na tuhabarishane na kulonga kwa habari zetu zipatikanazo katika jamii yetu ya TANZANIA na kote ulimwenguni,maana kama tutambuavyo kwamba kijana ni TAIFA la leo.Nchi yoyote ili uchumi wake uweze kukua na kuimarika ,unahitaji nguvu kazzi ya vijana kuweza kulisongesha jukumu la maendeleo ili  liweze kufika kule linakopaswa kufika.

Kama mwanaharakati wa vijana,nipo tayari kushirikiana na vijana wote kuweza kutoa mwanga katika jami yetu kwa mambo yanayotuzunguka vijana na kutetea haki za vijana,kielimu,maana kuna matatizo mbalimbali yawakumbayo vijana kielimu,na pia kiajira,kijana anapomaliza elimu yakeanakumbana na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira.

Lakini mimi kama mimi pekee yangu siwezi bali kama vijana tutakapoungana mikono na kushikana kwa pamoja ndipo tutakapoweza kumaliza matatizo yetu mbalimbali yanayotukabili sisi,kama vijana wa TAIFA la leo na si  taifa la kesho..

KIJANA NI TAIFA LA LEO,inabidi kijana ujitambue kwa kujua haki zako,na kupata habari za kila siku  ili tuweze kutokomeza tatizo la migomo  mbalimbali ya vijana,ukosefu wa ajira na kupanua uchumi wetu kwa kiwango kikubwa maana bila sisi vijana kujituma,hatutaweza kupigana na tatizo la umaskini linalotukabili.

KIJANA,amka na usome  habari za kukufanya uelimike na kuwa  kijana wa TAIFA la leo na ujitambue kuwa we ni wa leo na si wa kesho….NI HAPA HAPA kila siku ndani ya blog yako ya VIJANA TANZANIA……..KARIBUNI SANA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s