Nancy Sumari awa Mwandishi.


bookMwanadada aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2005 na kutwaa taji la Miss Africa mwaka huo huo Nancy Sumari, leo amezindua rasmi kitabu chake kinachokwenda kwa jina la ‘Nyota Yako’. Continue reading

Advertisements

Tuhuma za ‘UGAIDI’ zamfikisha mahakamani Lwakatare wa Chadema.


Rwakatare

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka manne likiwamo la kula njama ya kutaka kutoa sumu, kufanya mkutano wa ugaidi na kupanga tukio la kumteka nyara Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky. Continue reading

Hivi ndivyo kijana wa kisasa anapaswa kuwa


Tuangalie muonekano wao wa mavazi,tabia na vitu vingine ambavyo tunapaswa kujifunza

Muonekanao safi na wenye kupendeza ni sifa nzuri kwa kijana wa kisasa na inapaswa kijana kujitambua kuanzia mavazi,kiakili na hata kimawazo ndivyo vitu vinavyofanya kijana kuwa katika hali nzuri hata akienda sehemu kuacha watu wakiwa na hamu ya kuendelea kumtizama na kuwa naye karibu.

Kijana kutokuwa nadhifu,kujitambua na kuwa katika hali ya uchafu ni vitu ambavyo vinamshusha thamani kwa haraka sana,na wakati mwingine kijana anaweza kuwa na jambo la busara kusema katikati ya wenzake lakini ule muonekano wake ukasababisha watu washindwe kumheshimu katika jamii inayomzunguka. Continue reading

Dah!! Walimu vijana waililia serikali


Mazingira yasiyoridhisha ya kufundishia na kusomea kwa muda mrefu yamekuwa miongoni mwa kile kinachosemekana kuwa ni chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa kiwango cha elimu hapa nchini ambapo vijana wengi walimu ambao ndio wajenga taifa wamelazimika kufanya kazi katika mazingira magumu.

Ukosefu wa zana za kufundishia na kujifunzia ni pamoja na vitu kama uhaba mkubwa wa vitabu vya ziada na kiada, mazingira mabovu ya kuishi na kuna umbali mrefu walimu kuzifikia shule hizo na wao wenyewe wanadai kutokuwepo na mafunzo juu ya mabadiliko ya mitaala kunawapa wakati mgumu kuweza kuendana na mabadiliko katika sekta ya elimu . Continue reading

Afukuzwa kazi kisa ‘Facebook’!!


Kijana mfanyakazi wa kampuni moja ya mambo ya masoko hapa nchini (jina linahifadhiwa) anayejulikana kwa jina la Rashidi,amefukuzwa kazi, kisa ni mtandao wa kijamii wa facebook na twitter.

kijana huyo ambaye inasemekana kila siku amekuwa na ugomvi na bosi wake pamoja na wateja kwa kuchelewesha kazi zao kila siku,wateja hao waliamua kuungana na kwenda kulalamika kwa bosi hali iliyopelekea kijana huyo kusimamishwa kazi mda huo huo. Continue reading

Toa maoni yako hapa